Sunday, February 21, 2016

Besigye apinga matokeo ya uchaguzi Uganda.


Image copyrightAFP
Image captionBesigye ambaye amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake tangu siku ya Ijumaa
Mmoja wa wapinzani wakuu katika uchaguzi mkuu uliomalizika hivi punde nchini Uganda, Dkt Kizza Besigye, amekatalia mbali matokeo ya uchaguzi huo, uliofanyika siku ya Alhamisi.
Bw Besigye ambaye amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake tangu siku ya Ijumaa amesema kuwa raia nchini Uganda wameshuhudia ulaghai mkubwa mno wa uchaguzi mkuu, kuwahi kufanyika katika taifa hilo la mashariki mwa Afrika.
Kanali huyo mstaafu ameelezea uchaguzi huo kama usio halali na kuwa ni mapinduzi ya kijeshi.
Rais wa muda mrefu Yoweri Kaguta Museveni, alitangazwa mshindi.
Rais Museveni ameiongoza Uganda kwa muhula wa tano mtawalia.
Image copyright
Image captionMuseveni ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka thelathini sasa, alipata zaidi ya asilimia 61
Rais Museveni ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka thelathini sasa, alipata zaidi ya asilimia 61 ya kura huku Besigye akijipatia asilimia 35 ya kura.
Wachunguzi wa kimataifa wanasema kuwa uchaguzi huo uliandaliwa katika mazingara ya hofu na kudhalalishwa.

No comments:

Post a Comment