Wednesday, February 17, 2016

USAFIRI WA PIKIPIKI WAPIGWA MARUFUKU BUJUMBURA.


Image result for USAFIRI WA PIKIPIKI

Image copyright
Burundi imepiga marufuku pikipiki kuingia katikati mwa mji mkuu Bujumbura katika juhudi za kujaribu kupunguza mashambulio.
Pikipiki hutumiwa sana kusafirisha watu na mizigo Bujumbura lakini sasa zimekuwa zikitumiwa kutekeleza mashambulio, meya wa Bujumbura Freddy Mbonimpa anasema.
Mtu mmoja aliuawa Jumatatu wiki hii watu waliokuwa wameabiri pikipiki waliporusha guruneti tatu.
Usalama umeimarishwa mjini humo tangu kutoka kwa mashambulio hayo na polisi wanapekua watu na magari, shirika la habari la AFP linasema.
“Polisi wamegundua kwamba wahalifu hubeba guruneti wakitumia mabegu au vikapu,” Bw Mbonimpa anasema.
Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Prime Ndikumagenge anasema marufuku hiyo itaathiri sana watu wanaosafiri kutoka eneo moja hadi jingine mjini.
Huwezi kutoka kusini mwa mji hadi kaskazini bila kupitia katikati mwa mji, anasema.
Machafuko yalizuka nchini Burundi Aprili mwaka jana Rais Pierre Nkurunziza, ambaye amekuwa uongozini tangu 2005, alipotangaza kwamba angewania urais kwa muhula wa tatu.
Watu 400 wamefariki na wengine 240,000 kutorokea nchi jirani tangu wakati huo.

No comments:

Post a Comment