Wednesday, February 3, 2016

Zika: Ugonjwa walazimu TATA kubadili jina la gari lao


Image copyrightTATA
Image captionZika: Ugonjwa walazimu TATA kubadili jina la gari lao 'Zica'
Kampuni ya kutengeneza magari ya TATA imelazimika kutafuta jina mbadala ya magari yake chapa Zica kufuatia kuenea kwa ugonjwa mbaya unaolemaza ubongo unaoenea kote duniani unaoitwa Zika.
Kampuni hiyo yenye asili ya India inahofia magari hayo yatahusishwa na ugonjwa huo uliolipuka Kusini mwa Marekani.
Taarifa kutoka kwa kampuni hiyo inasema kuwa ''ni wajibu wake wa kibinadamu kufuta jina hilo la Zica''.
Sadfa ni kuwa gari hilo la Zica lilikuwa limeratibiwa kuzinduliwa Jumatano mjini New Delhi.
Tata inasema kuwa japo watazindua gari hilo chini ya nembo hiyo ''Zica'' itabadilishwa jina katika majuma machache yajayo.
Ugonjwa wa Zika unaenezwa na aina fulani ya mbu husababisha hali inayoitwa ''microcephaly'' ambayo inamaanisha kudumaa kwa fuvu la mtoto.
Image copyrightEPA
Image captionUgonjwa wa Zika unaenezwa na aina fulani ya mbu husababisha hali inayoitwa ''microcephaly'' ambayo inamaanisha kudumaa kwa fuvu la mtoto.
Tata ilifupisha ''Zippy Car'', ndio ikapata jina la gari hiyo mpya.
Tata ilitamba sana kwa magari yake ya NANO lakini pia inamiliki magari yenye nembo ya Jaguar na Land Rover.
Magari hayo ya Zica yamekuwa yakipigiwa debe kwa matangazo ya kibiashara yanayomjumuisha mshambulizi wa Argentina na Barcelona Lionel Messi.
Ugonjwa huu husababisha kichwa cha mtoto kusalia kidogo kuliko kawaida.
Hakuna dawa inayojulikana inayoweza kukinga ugonjwa huu wa Zika.
Takriban mataifa 20 yameathirika katika mlipuko huu wa Zika.
Wataalam wa maswala ya afya wa shirika la afya duniani, WHO wanahofu kuwa virusi vya Zika vinasambaa mbali na kwa haraka zaidi ,vikisababisha madhara makubwa.
Maambukizi yamekuwa yakihusishwa na maelfu ya watoto wanaozaliwa wakiwa na vichwa vidogo.
Tahadhari ya WHO kuhusu Zika ni ya hali ya juu sawa na ya Ebola
Image captionSadfa ni kuwa gari hilo la Zica lilikuwa limeratibiwa kuzinduliwa Jumatano mjini New Delhi.
Hii inamaanisha kuwa utafiti na msaada itatolewa kwa haraka kupambana na maambukizi.
Mkurugenzi mkuu wa WHO, Margaret Chan amesema nguvu ya pamoja inahitajika kupambana na virusi hivyo
Chan amesema masuala yanayopewa kipaumbele ni kuwalinda wanawake wajawazito na watoto dhidi ya mbu wanaosambaza virusi.
Tangu mwezi Oktoba kumekuwa na visa 4,000 za watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo kupita kiasi nchini Brazil pekee.

No comments:

Post a Comment