UN kutuma wataalamu Burundi kuchunguza makaburi yaliyozikwa watu wengi.
Umoja wa Mataifa unataka kutuma wataalamu huru wa wanaoweza kutambua alama za eneo la tukio nchini Burundi kuwasaidia maafisa wanaochunguza kuhusu makaburi yaliyozikwa watu wengi katika nchi hiyo iliyokumbwa na mzozo.
Baada ya ukandamizaji wa majeshi ya usalama nchini Burundi mwezi Desemba dhidi ya waandamanaji , watu walioshuhudia wamejitokeza na kutoa maelezo ya kuwapo kwa kiasi ya makaburi tisa yaliyozikwa watu wengi ndani na nje ya mji mkuu Bujumbura ikiwa ni pamoja na moja katika kambi ya jeshi.
Burundi imekuwa katika hali ya ghasia tangu rais Pierre Nkurunziza kutangaza mipango mwezi Aprili mwaka jana ya kuwania muhula wa tatu madarakani. Zaidi ya watu 400 wameuwawa katika ghasia na kiasi ya wengine 230,000 wameikimbia nchi hiyo.
Jana Jumatano Marekani iliishutumu Rwanda kwa kuhusika na vitendo vya kuidhoofisha nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na kuwaorodhesha wakimbizi kwa nia ya kuishambulia serikali ya Burundi.
No comments:
Post a Comment