Alshabab wadai kufanya shambulizi katika hoteli moja mjni Mogadishu.
Kiasi ya watu zaidi ya tisa wakiwemo raia wameripotiwa kuuawa nchini Somalia katika tukio lililohusisha mashambulizi ya risasi kati ya watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa kundi la itikadi kali la Al- Shabab na walinzi wa hoteli moja iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo , Mogadishu kabla ya vikosi vya usalama vya serikali kuingilia kati na kuzima shambulio hilo. Duru kutoka nchini humo zinaarifu kuwa kiasi ya wanamgambo watano waliuawa huku pia raia tisa wakidaiwa kuuawa katika tukio hilo. Mtu mmoja aliyekuwa amebeba miripuko katika gari alijiripua kwa kujitoa muhanga baada ya kuliingiza gari hilo kwa nguvu katika lango la hoteli hiyo ijulikanayo kama SYL hapo jana usiku na kutoa mwanya kwa watu waliokuwa na bunduki kutumia fursa hiyo kujaribu kulazimisha kupita katika kizuizi cha kwanza cha ulinzi ingawa washambuliaji hao hawakufanikiwa kupita katika kizuizi cha pili cha lango la hoteli hiyo. Washambuliaji wanne waliokuwa na bunduki pamoja na mtu aliyejitoa muhanga ni miongoni mwa waliouawa katika tukio hilo. Kundi la Al- Shababu limedai kuhusika na shambulizi hilo.
No comments:
Post a Comment