Tuesday, February 16, 2016


Image result for uganda
Mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa jana wakati waandamanaji nchini Uganda walipopambana na polisi kufuatia kukakamatwa kwa mgombea wa upinzani katika uchaguzi wa rais Kizza Besigye. Polisi imesema watu 20 walikamatwa katika maandamano hayo. Besigye, mpinzani mkuu wa Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi wa Alhamisi wiki hii, alikamatwa wakati akienda kuwahutubia maelfu ya wafuasi wake mjini Kampala. Alitumia barabara tofauti na ile aliyoruhusiwa na polisi, na hapo ndipo polisi wakafyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya wafuasi wake. Alizuiwa na kuachiwa huru muda mfupi baadaye. Hiyo ilikuwa mara ya pili Besigye kukamatwa kabla ya uchaguzi huo mkuu wa rais wa wabunge. Mgombea wa tatu mkuu upinzani Amama Mbabazi ambaye ni waziri mkuu wa zamani, pia aliwahi kukamatwa kwa muda mfupi.

No comments:

Post a Comment