Polisi Uganda yawarushia wapiga kura mabomu ya kutoa machozi.
Polisi wa Uganda wamefyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wapiga kura waliokuwa wamejawa na ghadhabu katika mji mkuu wa Uganda, Kampala. Wapiga kura wameghabishwa na kuchelewa kuanza kwa zoezi la upigaji kura katika vituo vingi mjini humo. Tume ya uchaguzi ya Uganda imeomba radhi kwa kuchelewa kufikishwa kwa makaratasi ya kupiga kura vituoni na kutoa wito wa kuwepo subira na utulivu wakati wa zoezi hilo.Tume hiyo imelazimika kuongeza muda wa zoezi hilo hadi saa moja jioni. Upigaji kura ulipaswa kuanza saa moja asubuhi saa za Afrika Mashariki lakini ulichelewa kwa saa kadhaa. Rais wa sasa Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani kuanzia mwaka 1986 anabashiriwa kushinda uchaguzi huo. Wagombea wengine wa urais ni Kizza Bessigye na aliyekuwa Waziri mkuu wa Uganda Amama Mbabazi.
No comments:
Post a Comment