Rais Obama kuzuru Cuba
Rais wa Marekani Barrack Obama anatarajiwa kufanya ziara nchini Cuba wiki ziijazo ikiwa miongoni mwa safari zake katika eneo la Kusini mwa Marekani,ripoti zinasema.
Atakuwa rais wa pili wa Marekani kusafiri katika kisiwa hicho ,baada ya Calvin Coolidge mwaka 1928.
Wanachama wa chama cha Republican nchini Marekani wameikosoa ziara hiyo wakisema haifai kufanyika wakati ambapo familia ya Castro ipo mamlakani.
Washington na Havana waliimarisha uhusiano wao mnamo mwezi Julai huku Marekani ikiondoa vikwazo vya kusafiri na vya kibiashara baada ya miaka 54.
Mgombea wa uraisi nchini Marekani kupitia tiketi ya chama cha Republican Marco Rubio na Ted Crus,wote wakiwa watoto wa wahamiaji wa Cuba walisema kuwa ziara hiyo haifai na ni makosa makubwa.
Alipoulizwa iwapo angesafiri nchini Cuba,Bwana Rubio alisema kuwa ni taifa ambalo haliko huru.
Bwana Crus alisema kwamba bwana Obama ataonekana kama ''anayomba msamaha''.
Mnamo mwezi Disemba,Obama aliliambia shirika la habari la Yahoonews kwamba alitaka kukutana na wapinzani wa kisiasa nchini Cuba ili kusaidia kuisukumu serikali ya Cuba katika mwelekeo mwema.
No comments:
Post a Comment