Monday, February 8, 2016


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani hatua ya Korea ya Kaskazini  ya jaribio la kombora la masafa marefu ambalo viongozi wa dunia wanasema ni teknolojia iliyopigwa marufuku na kusema ni kitendo cha uchokozi kisichoweza kuvumiliwa. Baraza hilo la usalama la Umoja wa Mataifa linakusudia kupitisha azimio jipya  haraka iwezekanavyo litakaloendana na hatua ya vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini. Korea Kaskazini imefanya jaribio la kombora hilo ikiwa ni mwezi mmoja tu umepita tangu ilipofanya jaribio lingine la nne la kombora la nyukilia na kukiuka wito uliotolewa na nchi jirani ya China  na ambayo ni mshirika wake mkubwa  ya kutoendelea na majaribio hayo ya makombora ya masafa marefu. Tangu Januari 6, mwaka huu Korea Kaskazini ilipofanya jaribio la kombora la masafa marefu ambalo ilidai kuwa ni kombora kali la bomu la Haidrojeni , mataifa ya China na Marekani yamekuwa yakijadiliana juu ya azimio jipya la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakaloibana Korea Kaskazini kuendelea na majaribio hayo.

No comments:

Post a Comment