Uturuki yaapa kulipiza kisasi shambulio.
Uturuki imeapa kulipiza kisasi dhidi ya washambuliaji wa mlipuko mkubwa wa bomu katika mji mkuu wa Ankara,ambao umewawacha watu 28 wakiwa wamefariki na wengine 61 wakijeruhiwa.
''Uturuki haitaogopa kutumia uwezo wake wa kujilinda,rais Recep Tayyip Erdogan amesema.
Maafisa wamesema kuwa gari lililojaa vilipuzi lililipuliwa wakati ambapo mabasi ya jeshi yalikuwa yakipita siku ya jumatano.Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Alamisi.
Hakuna kundi lolote kufikia sasa lililodai kutekeleza shambulio hilo.
Marekani ilishtumu mlipuko huo ,huku msemaji wa baraza la usalama wa kitaifa Ned Price akisema,tunasimama pamoja na Uturuki ,mshirika wa Nato na mshirika wetu mkuu.
Mlipuko huo ulitokea katika eneo la karibu na bunge na makao makuu ya jeshi.
Moshi mkubwa ulionekana ukifuka kutoka eneo hilo na mashahidi wanasema mlipuko huo ulisikika mji mzima.
No comments:
Post a Comment