Monday, June 27, 2016

PICHA TATU ZA KITWANA AKIKABIDHI OFISI.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amekabidhiwa ofisi rasmi na  aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo.
????????????????????????????????????

1

Magufuli awateua wakuu 100 wa wilaya


Image captionMagufuli awateua wakuu wapya wa wilaya 100
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewafuta kazi wakuu wawili wa mikoa.
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela na mwenzake wa Mara Bw. Stanslaus Magesa Mulongo wamefutwa kazi.
Katika nafasi zao rais Magufuli amewateua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Aidha Bi. Zainab R. Telack amehamishwa na kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Vilevile Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
''Walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi'' taarifa hiyo kwa vyombo vya habari inasema.
Na katika hatua ya kipekee rais Magufuli amewastaafisa maafisa wakuu wa wilaya waliohitimu miaka 60.
Bwana Magufuli aliwateua wakuu wa wilaya 139.
Wakuu wa Wilaya waliosalia madarakani ni 39 pekee.
''Nafasi 78 za uteuzi wa wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali''.
Taarifa hiyo ya ikulu iliyotiwa sahihi na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano, ikulu Gerson Msigwa inaongezea
Orodha kamili ya walioteuliwa ni kama ifuatavyo.
ARUSHA
Arusha - Mrisho Mashaka Gambo
Arumeru - Alexander Pastory Mnyeti
Ngorongoro - Rashid Mfaume Taka
Longido - Daniel Geofrey Chongolo
Monduli - Idd Hassan Kimanta
Karatu - Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM
Kinondoni - Ally Hapi
Ilala - Sophia Mjema
Temeke - Felix Jackson Lyaviva
Kigamboni - Hashim Shaibu Mgandilwa
Ubungo - Hamphrey Polepole
DODOMA
Chamwino - Vumilia Justine Nyamoga
Dodoma - Christina Solomon Mndeme
Chemba - Simon Ezekiel Odunga
Kondoa - Sezeria Veneranda Makutta
Bahi - Elizabeth Simon
Mpwapwa - Jabir Mussa Shekimweli
Kongwa - John Ernest Palingo
GEITA
Bukombe - Josephat Maganga
Mbogwe - Matha John Mkupasi
Nyang'wale - Hamim Buzohera Gwiyama
Geita - Herman C. Kipufi
Chato - Shaaban Athuman Ntarambe
IRINGA
Mufindi - Jamhuri David William
Kilolo - Asia Juma Abdallah
Iringa - Richard Kasesela
KAGERA
Biharamulo - Saada Abraham Mallunde
Karagwe - Geofrey Muheluka Ayoub
Muleba - Richard Henry Ruyango
Kyerwa - Col. Shaban Ilangu Lissu
Bukoba - Deodatus Lucas Kinawilo
Ngara - Lt. Col. Michael M. Mtenjele
Missenyi - Lt. Col Denis F. Mwila
KATAVI
Mlele - Rachiel Stephano Kasanda
Mpanda - Lilian Charles Matinga
Tanganyika - Saleh Mbwana Mhando
KIGOMA
Kigoma - Samsoni Renard Anga
Kasulu - Col. Martin Elia Mkisi
Kakonko - Col. Hosea Malonda Ndagala
Uvinza - Mwanamvua Hoza Mlindoko
Buhigwe - Col. Elisha Marco Gagisti
Kibondo - Luis Peter Bura
KILIMANJARO
Siha - Onesmo Buswelu
Moshi - Kippi Warioba
Mwanga - Aaron Yeseya Mmbago
Rombo - Fatma Hassan Toufiq
Hai - Gelasius Byakanwa
Same - Rosemary Senyamule Sitaki
LINDI
Nachingwea - Rukia Akhibu Muwango
Ruangwa - Joseph Joseph Mkirikiti
Liwale - Sarah Vicent Chiwamba
Lindi - Shaibu Issa Ndemanga
Kilwa - Christopher Emil Ngubiagai
MANYARA
Babati - Raymond H. Mushi
Mbulu - Chelestion Simba M. Mofungu
Hanang' - Sara Msafiri Ally
Kiteto - Tumaini Benson Magessa
Simanjiro - Zephania Adriano Chaula
MARA
Rorya - Simon K. Chacha
Serengeti - Emile Yotham Ntakamulenga
Bunda - Lydia Simeon Bupilipili
Butiama - Anarose Nyamubi
Tarime - Glodious Benard Luoga
Musoma - Dkt. Vicent Anney Naano
MBEYA
Chunya - Rehema Manase Madusa
Kyela - Claudia Undalusyege Kitta
Mbeya - William Ntinika Paul
Rungwe - Chalya Julius Nyangidu
Mbarali - Reuben Ndiza Mfune
MOROGORO
Gairo - Siriel Shaid Mchembe
Kilombero - James Mugendi Ihunyo
Mvomero - Mohamed Mussa Utali
Morogoro - Regina Reginald Chonjo
Ulanga - Kassema Jacob Joseph
Kilosa - Adam Idd Mgoyi
Malinyi - Majula Mateko Kasika
MTWARA
Newala - Aziza Ally Mangosongo
Nanyumbu - Joakim Wangabo
Mtwara - Dkt. Khatibu Malimi Kazungu
Masasi - Seleman Mzee Seleman
Tandahimba - Sebastian M. Walyuba
MWANZA
Ilemela - Dkt. Leonald Moses Massale
Kwimba - Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
Sengerema - Emmanuel Enock Kipole
Nyamagana - Mary Tesha Onesmo
Magu - Hadija Rashid Nyembo
Ukerewe - Estomihn Fransis Chang'ah
Misungwi - Juma Sweda
NJOMBE
Njombe - Ruth Blasio Msafiri
Ludewa - Andrea Axwesso Tsere
Wanging'ombe - Ally Mohamed Kassige
Makete - Veronica Kessy
PWANI
Bagamoyo - Alhaji Majid Hemed Mwanga
Mkuranga - Filberto H. Sanga
Rufiji - Juma Abdallah Njwayo
Mafia - Shaibu Ahamed Nunduma
Kibaha - Asumpter Nsunju Mshama
Kisarawe - Happyness Seneda William
Kibiti - Gulamu Hussein Shaban Kifu
RUKWA
Sumbawanga - Dkt. Khalfan Boniface Haule
Nkasi - Said Mohamed Mtanda
Kalambo - Julieth Nkembanyi Binyura
RUVUMA
Namtumbo - Luckness Adrian Amlima
Mbinga - Cosmas Nyano Nshenye
Nyasa - Isabera Octava Chilumba
Tunduru - Juma Homela
Songea - Polet Kamando Mgema
SHINYANGA
Kishapu - Nyambonga Daudi Taraba
Kahama - Fadhili Nkulu
Shinyanga - Josephine Rabby Matiro
SIMIYU
Busega - Tano Seif Mwera
Maswa - Sefu Abdallah Shekalaghe
Bariadi - Festo Sheimu Kiswaga
Meatu - Joseph Elieza Chilongani
Itilima - Benson Salehe Kilangi
SINGIDA
Mkalama - Jackson Jonas Masako
Manyoni - Mwembe Idephonce Geofrey
Singida - Elias Choro John Tarimo
Ikungi - Fikiri Avias Said
Iramba - Emmanuel Jumanne Luhahula
SONGWE
Songwe - Samwel Jeremiah
Ileje - Joseph Modest Mkude
Mbozi - Ally Masoud Maswanya
Momba - Juma Said Irando
TABORA
Nzega - Geofrey William Ngudula
Kaliua - Busalama Abel Yeji
Igunga - Mwaipopo John Gabriel
Sikonge - Peres Boniphace Magiri
Tabora - Queen Mwashinga Mlozi
Urambo - Angelina John Kwingwa
Uyui - Gabriel Simon Mnyele
TANGA
Tanga - Thobias Mwilapwa
Muheza - Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
Mkinga - Yona Lucas Maki
Pangani - Zainab Abdallah Issa
Handeni - Godwin Crydon Gondwe
Korogwe - Robert Gabriel
Kilindi - Sauda Salum Mtondoo
Lushoto - Januari Sigareti Lugangika
Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wataapishwa Jumatano.

Rais wa Senate na naibu wake wafikishwa mahakani Nigeria


Image captionBukola Saraki
Rais wa Bunge la Senate nchini Nigeria na naibu wake wamefikishwa mbele ya mahakama kwa makosa ya kugushi, ambayo ina adhabu kali hasa kwa kuwa wao ni wanasiasa watajika nchini humo.
Bukola Saraki na naibu wake Ike Ekweremadu, wamekanusha madai hayo yanayoaminika kutekelezwa mwaka jana, ambayo iliwasaidia kupata vyeo walivyo navyo sasa.
Iwapo watapatikana na hatia, watahukumiwa kifungo cha hadi miaka 14 jela.
Bwana Saraki pia, amekuwa akikabiliwa na kesi nyingine mahakamani kuhusiana na udanganyifu wa mali anayodaiwa kumiliki, makosa ambayo ameyakanusha.

Uturuki yaiomba Urusi msamaha


Image copyrightREUTERS
Image captionErdogan
Urusi inasema kuwa Rais Erdogan wa Uturuki ameomba msamaha kwa hatua ya taifa lake, kuidungua ndege ya kivita ya Urusi karibu na mpaka na Syria mwaka jana.
Katika ujumbe ulioandikwa ndani ya barua hadi Kremlin kwa Rais Putin, Bwana Erdogan alielezea masikitiko yake makubwa kwa kile kilichofanyika, huku akisema anataka kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.
Image copyrightREUTERS
Image captionNdege ya Urusi iliyodunguliwa
Uturuki bado haijatoa maelezo kuhusiana na barua hiyo.
Udunguaji wa ndege hiyo uliibua mgongano mkubwa wa kisiasa, uliopeleekea Urusi kuiwekea Uturuki vikwazo vya kibiashara ambavyo vingeondolewa tu baada ya Rais Erdogan kuomba msamaha.

Wanajeshi wa AMISOM hawajalipwa kwa miezi sita


Image copyrightREUTERS
BBC imebaini kuwa wanajeshi wa AMISON wanapigana vita na kundi la al shabab nchini Somalia hawajalipwa marupuru yao kwa miezi sita.
Kikosi hicho cha AMISOM kinafadhiliwa na Muungano wa Ulaya.
Taarifa za EU ziliiambia BBC kuwa malipo hayo ya miezi sita, yamezuiwa kutokana na matatizo ya kiuhasibu.
EU inastahili kumlipa dola 1000 kwa kila mwanajehsi wa AMISON kila mwezi.

Rais Zuma aamrishwa kurejesha pesa za Umma.


Image copyright
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameambiwa kuwa ni lazima alipe zaid ya dola nusu milioni pesa za umma, ambazo alitumia kukarabati nyumba yake.
Mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini imetaka wizara ya fedha, kutambua ikiwa ni kiaisi gasi Rais Zuma anasathili kurejesha kufutia uamuzi wa mapema mwaka huu kuwa alikuwa amekiuka katiba
Image copyrightREUTERS
Image captionMakao ya Zuma ya Nkandla
Kumekuwa na wito wa kumtaka Raia Zuma ajiuzulu kutokana na sakata hiyo.

Wednesday, June 22, 2016

KITWANGA AREJEA KUTOKA ISLAEL (hii ni kutoka millard ayo.com)
Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.
Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha habari ‘Kitwanga: Yaliyotokea namwachia Mungu, asema amerudi na nguvu mpya, kutua bungeni wiki ijayo’


 Kitwanga asema yuko imara na amerejea nchini akiwa na nguvu mpya, ajipanga kufanya kazi usiku na mchana
Gazeti la Mtanzania limeripoti kuwa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi,Charles Kitwanga amesema yupo imara na amerejea nchini akiwa na matumaini mapya, pamoja na hali hiyo, amesema kuwa hivi sasa anajipanga kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha anasaidia nchi pamoja na wapigara wake na maendeleo ya kweli.
Kauli hizo alizitoa Dar es salaam jana alipozungumza na Gazeti la Mtanzania katika mahojiano maalumu baada ya kurejea akitokea nchini Israel  ambako alikwenda kwa shughuli zke binafsi, Gazeti hilo limemnukuu akizungumza haya………
>>>’niko imara kabisa na nina nguvu na matumaini mapya, nimeingia nchini juzi nikitokea nchini Israel ambako nilikuwa na shughuli zangu binafsi, unajua mimi ni mtaalamu (wa mawasiliano) na wewe unajua kabla sijaingia kwenye siasa nilikuwa nafanya nini’.

>>>’kifupi nasema nilikwenda Israel kwa shughuli zangu binafsi kabisa ambazo kwa kipindi cha wiki tatu nilizokuwa huko nimefanya. hata wanaosema nilikwenda kulia kwa Bwana nao ni mawazo yao, maana unajua ile ni nchi takatifu kutokana na historia yake’.