Rais wa Senate na naibu wake wafikishwa mahakani Nigeria
Rais wa Bunge la Senate nchini Nigeria na naibu wake wamefikishwa mbele ya mahakama kwa makosa ya kugushi, ambayo ina adhabu kali hasa kwa kuwa wao ni wanasiasa watajika nchini humo.
Bukola Saraki na naibu wake Ike Ekweremadu, wamekanusha madai hayo yanayoaminika kutekelezwa mwaka jana, ambayo iliwasaidia kupata vyeo walivyo navyo sasa.
Iwapo watapatikana na hatia, watahukumiwa kifungo cha hadi miaka 14 jela.
Bwana Saraki pia, amekuwa akikabiliwa na kesi nyingine mahakamani kuhusiana na udanganyifu wa mali anayodaiwa kumiliki, makosa ambayo ameyakanusha.
No comments:
Post a Comment