Sunday, June 19, 2016

Wanamgambo 8 wauawa Algeria.


Jeshi la Algeria linasema kuwa limewaua wanamgambo 8 kusini mwa mji mkuu Algiers.
Jeshi lilisema kuwa silaha na risasi pia vilipatikana wakati wa oparesheni hiyo iliyofanyika katika eneo la milima la Madea.
Taarifa za kijeshi hazikusema ni kundi lipi wanamgambo hao walitoka.
Lakini wapiganaji kutoka makundi ya Al Qaeda na Islamic State wamekuwa wakiendesha shughuli zao maeneo ya vijiji mbali mwa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment