Sunday, June 19, 2016

Muuza vitabu wa Hong Kong alifikiria kujiua.


Image copyrightEPA
Image captionLam Wing-kee
Muuza vitabu wa Hong Kong, ambaye alikamatwa na wakuu wa Uchina, ameiambia BBC, kwamba alifikiria kujiua.
Lam Wing-kee alisema, aliteswa sana kiakili, alipofungwa kwa miezi minane.
Ameshawahi kusema, kwamba alilazimishwa kutia saini, kukubali kuwa hana haki ya kumuona wakili.
Bwana Lam, mmoja kati ya wauza vitabu watano, ambao walifungwa Uchina, alirudi Hong Kong juma lilopita, kufichua yaliyomkuta gerezani.
Watu wengi wanaamini kuwa watu hao watano walikamatwa, kwa sababu wakiuza vitabu kuhusu viongozi wa Uchina.

No comments:

Post a Comment