Sunday, June 19, 2016

Algeria yafunga mitandao kuzuia udanganyifu kwenye mitihani.


Algeria imefunga kwa muda mitandao ya kijamii kote nchini katika jitihada za kuzuia wizi wa mitihani ya shule za upili.
Karibu nusu ya wanafunzi walilazimishwa kurudia mtihani huo kuanzia leo Jumapili, baada ya mtihani wa kwanza kukumbwa na udanganyifu kwa njia ya mitandao.
Wanafunzi wengi walifanikiwa kupata maswali kwa njia ya mtandao wa Facebook na mitandao mingine kabla ya kufanyika kwa mtihani huo.
Hatua ya kufunga mitandao ya kijamii ililenga kuwalinda wanafunzi kutokana na kuchapisha maswali yasiyo sahihi kupitia kwa mitandao hiyo.

No comments:

Post a Comment