UNHCR: Watu milioni 65 ni wakimbizi.
Shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi, UNHCR linasema kuwa idadi ya watu ambao wameondolewa makwao kwa sababu ya mizozo, imepanda maradufu kuliko wakati mwingine ule.
Katika ripoti yake ya kila mwaka inayohusiana na rekodi ya watu wanaofurushwa makwao- UNHCR inasema kwamba, kufikia mwishoni mwa mwaka jana, zaidi ya watu milioni 65 kote duniani, au mtu mmoja kati ya 113 katika sayari hii ni mkimbizi, mhamiaji au wakimbizi wa ndani kwa ndani.
Zaidi ya nusu ya wakimbizi hao wote wanatoka nchini Syria, Afghanistan na Somalia.
Umoja wa mataifa unasema kuwa, serikali za dunia zinafaa kuonyesha umoja na mshikamano kuhusiana na swala hilo tata- sio tu kwa ajili ya wakimbizi, lakini katika swala nzima ya kulinda jamii ya dunia.
No comments:
Post a Comment