Muhubiri anayetaka wapenzi wa jinsia moja kuuawa aondoka Australia.
Muhubiri mmoja wa kiislamu ambaye alisema kwamba wapenzi wa jinsia moja wanafaa kuuawa ameondoka nchini Australia.
Kiongozi huyo ambaye ni mzaliwa wa Uingereza Farrokh Sekaleshfar alikuwa mwalimu katika shule moja karibu na Orlando ,Florida mnamo mwezi Aprili an alinukuliwa akitoa matamshi hayo siku moja kabla ya shambulio la Orlando.
Alikuwa amezuru Australia kama mgeni wa Imam Hussein wa kituo cha kiislamu cha Sidney.
Vyombo vya habari viliripoti siku ya Jumatano kwamba Sheikh Sekaleshfar aliondoka nchini humo baada ya waziri mkuu Malcom Turnbull kutaka visa yake ichunguzwe.
Waziri wa Australia Peter Dutton amesema kuwa alifutilia mbali visa ya Sekaleshfar na kwamba itakuwa vigumu kurudi nchini humo.
Lakini bw Dutton ametetea idara yake dhidi ya madai kwamba visa ya kiongozi huyo wa dini haifai kuidhinishwa.
No comments:
Post a Comment