Wednesday, June 22, 2016

Ashtakiwa kumtusi Magufuli katika WhatsApp


Image captionMagufuli
Raia mmoja wa Tanzania amefunguliwa mashtaka kutokana na ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa WhatsApp ambapo anadaiwa kumtusi Rais John Pombe Magufuli.
Mulokozi Kyaruzi ameshtakiwa chini sheria uhalifu wa mtandaoni.
Ni mtu wa pili kushtakiwa chini ya sheria hiyo kwa tuhuma za kumtusi rais.
Sheria hiyo ilikosolewa sana kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza wakati ilipoanza kutekelezwa mwaka uliopta.
Kyaruzi anadaiwa kuandika: "'Kwani rais Magufuli hana washauri? hashauriki? Ama ni mjinga tu? Ni Mpumbavu sana. Haangalii sheria iliopo kabla ya kufungua mdomo ama anaugua ugonjwa wa Mnyika''?.

No comments:

Post a Comment