Ufaransa kuongeza ulinzi katika michezo ya Euro 2016.
Ufaransa itaimarisha ulinzi katika michezo ya kandanda ya kombe la mataifa ya Ulaya, Euro 2016, ikiweka zaidi ya polisi 1,000 wa ziada na wanajeshi.
Hatua hizo za ziada zilitangazwa wakati Ukraine imesema imemkamata Mfaransa anayeshukiwa kupanga mashambulizi kadhaa ya kigaidi wakati wa michezo hiyo.
Kwa jumla , zaidi ya polisi 90,000 , na wanajeshi pamoja na wakala wa usalama watakuwapo kwa muda wote wa mashindano hayo yatakayodumu kwa mwezi mzima na yanaanza rasmi siku ya Ijumaa.
Naibu meya wa jiji la Paris Jean Francois Martins amesema kila kitu kiko tayari kwa mashindano hayo.
Kiasi ya mashabiki milioni 1.5 wanatarajiwa kuhudhuria mashindano hayo yatakayokuwa na michezo 51 katika viwanja 10 nchini Ufaransa.
No comments:
Post a Comment