KITWANGA AREJEA KUTOKA ISLAEL (hii ni kutoka millard ayo.com)
Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.
Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha habari ‘Kitwanga: Yaliyotokea namwachia Mungu, asema amerudi na nguvu mpya, kutua bungeni wiki ijayo’
#MTANZANIA Kitwanga asema yuko imara na amerejea nchini akiwa na nguvu mpya, ajipanga kufanya kazi usiku na mchana
Gazeti la Mtanzania limeripoti kuwa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi,Charles Kitwanga amesema yupo imara na amerejea nchini akiwa na matumaini mapya, pamoja na hali hiyo, amesema kuwa hivi sasa anajipanga kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha anasaidia nchi pamoja na wapigara wake na maendeleo ya kweli.
Kauli hizo alizitoa Dar es salaam jana alipozungumza na Gazeti la Mtanzania katika mahojiano maalumu baada ya kurejea akitokea nchini Israel ambako alikwenda kwa shughuli zke binafsi, Gazeti hilo limemnukuu akizungumza haya………
>>>’niko imara kabisa na nina nguvu na matumaini mapya, nimeingia nchini juzi nikitokea nchini Israel ambako nilikuwa na shughuli zangu binafsi, unajua mimi ni mtaalamu (wa mawasiliano) na wewe unajua kabla sijaingia kwenye siasa nilikuwa nafanya nini’.
>>>’kifupi nasema nilikwenda Israel kwa shughuli zangu binafsi kabisa ambazo kwa kipindi cha wiki tatu nilizokuwa huko nimefanya. hata wanaosema nilikwenda kulia kwa Bwana nao ni mawazo yao, maana unajua ile ni nchi takatifu kutokana na historia yake’.
No comments:
Post a Comment