Monday, June 13, 2016

Euro 2016: Marufuku ya pombe viwanjani


Image copyrightGETTY
Image captionUlevi unatajwa kuwa ni moja ya vyanzo vya vurugu hizo
Waziri wa maswala ya ndani wa ufaransa , Bernard Cazeneuve, ametoa ushauri kwa wakuu wa miji mbalimbali wenyeji wa kinyanganyiro cha soka barani ulaya Euro2016, kupiga marufuku matumizi ya pombe katika maeneo tete siku ya na hata kabla ya siku ya mechi kufanyika.
Image copyrightEPA
Image captionWenye mabaa watalazimika kubadilisha mikebe na chupa wanayouzia pombe ilikuzuia madhara yanayotokana na walevi kutumia vyombo hivyo kama makombora
Hii ni kutokana na matukio ya wafuasi wa timu kadhaa kushambuliana katika visa vilivyochochewa na ulevi huko mjini Marseille katika kipindi cha siku 3 zilizopita.
Shirikisho la kandanda barani ulaya , UEFA, limeonya kuzichukulia hatua ya hata kuwafurusha kutoka mashindano hayo timu za Uingereza na Urusi iwapo mashabiki wao watajihusisha tena na matukio ya ghasia kama ilivyotokea wakati wa mechi yao katika mji wa Marseille .
Image copyrightREUTERS
Image captionUlevi unatajwa kuwa ni moja ya vyanzo vya vurugu hizo
Ulevi unatajwa kuwa ni moja ya vyanzo vya vurugu hizo ambapo baadhi ya mashabiki wana kwenda katika viwanja vya michezo wakiwa wamelewa chopi.
Serikali ya Uingereza tayari imeahidi kutuma idadi kubwa ya maaskari wa kupambana na fujo kabla ya mechi ijayo inayohusisha timu ya Uingereza siku ya Alhamisi.
Bwana Cazeneuve amenukuliwa akisema
Image copyrightGETTY
Image captionUingereza tayari imeahidi kutuma idadi kubwa ya maaskari wa kupambana na fujo kabla ya mechi ijayo inayohusisha timu ya Uingereza siku ya Alhamisi.
''Tutafanya kila tuwezalo kuzuia ghasia na machafuko zaidi ikiwemo kuzuia uuzaji wa pombe unywaji wa pombe na hata usafirishaji wa pombe kuelekea maneo wenyeji wa kombe la Euro''
''Tutaweka marufuku ya pombe katika maeneo yote ya umma''
Image copyrightAP
Image captionEuro 2016: Marafuku ya pombe viwanjani
Vilevile baa na migahawa inayouza tembo italazimika kubadilisha mikebe na chupa wanayouzia pombe ilikuzuia madhara yanayotokana na walevi kutumia vyombo hivyo kama makombora haswa dhidi ya polisi''
alisema bwana Cazeneuve.

No comments:

Post a Comment