Babake Reeva amtaka Pistorius kulipia alichotenda.
Baba wa mwanamitindo wa Afrika Kusini ambaye aliuawa Reeva Steenkamp, amezungumza mahakamani kwa mara ya kwanza akisema kuwa muuaji wa Reva, Oscar Pistorius lazima alipie yale aliyoyatenda.
Akizungumza mahakamani huku amejawa na majonzi, bwana Steenkamp alisema kuwa familia yake imetaabika kutokana na kuuawa kwa Reeva.
Alisema anaamini kuwa bintiye alikuwa amegombana na Oscar Pistorius usiku ambao aliuawa miaka mitatu iliyopita.
Bwana Steenkamp wakati huo hakuwa na afya nzuri kuweza kuhudhuria kesi.
Mahakama mjini Pretoria itaamua hukumu ambayo itampa Oscar baada ya hukumu ya kwanza kubadilishwa na kuwa mauaji.
No comments:
Post a Comment