Thursday, June 2, 2016


Mchezaji soka nyota wa Argentina Lionel Messi ambaye ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa kiwango kikubwa kabisa cha fedha amefika hii leo katika mahakama ya Barcelona kusimama kizimbani kwa mara ya kwanza katika kesi inayomkabili kuhusiana na suala la ukwepaji kulipa kodi nchini Uhispania. Messi mwenye umri wa miaka 28 ambaye ameonekana akiwa amevalia suti nyeusi alishangiliwa na mashabiki wakati akitoka ndani ya gari akiwa anaandamana na baba yake Jorge Horacio Messi. Messi na baba yake wanatuhumiwa kutumia msururu wa makampuni hewa huko Belize na Uruguay ili kukwepa kulipia kodi kipato cha Messi cha yuro milioni 4.6 alichokipata kupitia mauzo ya matangazo ya biashra kupitia jina lake kati ya mwaka 2007 hadi mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment