Sudan yawafukuza raia 442 wa Eritrea.
Serikali ya Sudan imewafurusha takriban raia 442 wa Eritrea ikiwemo wakimbizi sita waliosajiliwa kurudi nchini mwao mwezi huu kulingana na kundi moja la haki za kibinaadamu la Human Rights Watch.
''Sudan inawakamata na kuwalazimisha raia wa Eritrea kurudi katika serikali yao ilio na ukandamizaji bila kuwaruhusu wakimbizi kutafuta mahala pa kujilinda,alisema Gerry Simpson'',mkimbizi mwandamizi anayehusika na maswala ya utafiti katika HRW.
Sudan inafaa kufanya kazi na shirika la umoja wa mataifa kuhusu Ukimbizi ili kuwalinda,badala ya kuwarudisha nyumbani ili wakumbane na unyanyasaji,aliongezea.
Sudan haijatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.