Tuesday, May 31, 2016

Mgogoro kuhusu sherehe ya siku ya uhuru Kenya.


Image captionViongozi wa Upinzani nchini Kenya
Mahakama kuu nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi wake iwapo muungano wa upinzani nchini Kenya CORD utaendelea na mkutano wao hapo kesho katika sherehe za Madaraka.
Hivi majuzi muungano huo wa upizani uliandamana ukishinikiza maafisa wakuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) kujiuzulu.
Maandamano hayo yalishuhudia vifo vya watu kadha na polisi kutumia nguvu kupita kiasi.
Muungano wa Cord umesema ulitaka kutumia siku hiyo kama siku ya kutafakari.
Image captionMaandamano ya Upinzani Kenya
Baraza la Taifa la Ushauri la Usalama limetoa tahadhari kwamba mikutano ya kisiasa katika jiji la Nairobi, linatishia usalama wa kitaifa.
Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuwahutubia watu siku hiyo ya madaraka mjini Nakuru magharibi mwa Kenya.

No comments:

Post a Comment