Dharuba yasababisha maafuriko na watu 3 kufariki kusini magharibi mwa Ujerumani.
Dharuba na mvuwa kubwa zimesababisha mafuriko na watu watatu kufariki dunia katika jimbo la kusini magharibi mwa Ujerumani. Askari mmoja wa kikosi cha kukabiliana na maafa katika mji wa Schwäbisch Gmünd pamoja na mtu aliyekuwa akitaka kumuokoa ni miongoni mwa waliopoteza maisha, kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya jimbo la Baden-Württemberg. Katika mji wa Weißbach karibu na Heilbronn mtu mmoja amekufa maji baada ya kuzama akiwa ndani ya gereji ya chini ya nyumba yake. Dharuba na mvuwa kubwa zimepelekea kima cha mito kupanda sana na haraka katika eneo hilo. Magari mengi yamefunikwa na maji na vikosi vya uokozi vimelazimika kuwaokoa watu kadhaa waliokwama ndani ya magari yao. Mvuwa kubwa na dharuba zimesababisha hasara kubwa pia katika mikoa ya Ansbach na Neustadt/Aisch katika jimbo la kusini la Bavaria.
No comments:
Post a Comment