Liverpool, kupambana na Sevilla fainali.
Klabu ya Liverpool ya Uingereza itapambana na Servilla ya Uhispania katika fainali ya ligi ya Ulaya , Europa League, itakayofanyika katika mji wa Basel nchini Uswisi mwezi huu.
Klabu hiyo ya Uingereza ilizidi ngumu timu hiyo ya Uhispania jana usiku nyumbani, na kuishinda kwa mabao 3-0 katika mkondo wa pili wa nusu fainali na kushinda kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya michezo miwili.
Katika nusu fainali nyingine , Sevilla iliishinda Shaktar Donetsk kwa mabao 3-1 nyumbani na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-3.
Timu hizo mbili zitapambana katika fainali mjini Basel Mei 18, ambapo mshindi moja kwa moja anapata nafasi ya kucheza katika Champions League.
Sevilla, ikiwa ya saba katika msimamo wa ligi ya Uhispania, italenga kupata taji la tatu mfululizo la Ligi ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment