Monday, May 30, 2016

Jeshi la Iraq laanza kukomboa mji wa falluja.


Image copyrightAFP
Image captionWanajeshi wa Iraq
Wanajeshi wa Iraq wameanza kile wanachokitaja kama mashambulio ya mwisho kabisa ya kuukomboa mji wa Fallujah, kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Islamic State.
Fallujah ni mji ulioko kilomita 50 kutoka mji wa Baghdad, na umekuwa chini ya udhibiti wa IS kwa miaka miwili iliyopita.
Image copyrightAFPGETTY IMAGES
Image captionWanajeshi wa Iraq
Taarifa kutoka kwa idara ya usalama nchini Iraq, zinasema kuwa mapigano makali yamekuwa yakiendelea huko, tangu saa kumi na moja leo alfajiri.
Shambulio la hivi punde zaidi lilitekelezwa na kikosi maalum cha serikali cha kupambana na ugaidi, huku kikisaidiwa na majeshi ya muungano chini ya Marekani.
Image copyrightAFP
Image captionIslamic State
Yanashambulia Fallujah kutoka maeneo tatu tofauti, ili kuuzingira na kuziba kabisa njia za kukumbilia kwa wapiganaji hao wa IS.

No comments:

Post a Comment