Utoaji mimba wapigiwa kura Marekani.
Wanasiasa nchini Marekani katika jimbo la Oklahoma wamepiga kura kwa lengo la kufanya kitendo cha utoaji mimba kuwa kosa la jinai.
Hatua hiyo inaweza kuwaadhibu madaktari ambao mimba wamekuwa wakisaidia utoaji wa mimba kifungo cha miaka mitatu gerezani sambamba na kuwafungia vibali vya kufanya kazi.
Seneti wa jimbo hilo imekubali kupitishwa miswada kwa kura 33 kati ya12 na sasa itapaswa kuidhinishwa na gavana wa Republican katika jimbo hilo.
Mwandishi wa BBC aliyeko Kaskazini mwa Marekani amesema kuwa hata kama muswada huo utakuwa sheria, itakutana na changamoto katika mahakama ya juu sambamba na wanaharakati wanaokubaliana na suala la utoaji mimba.
Oklahoma ni jimbo la mwisho nchini humo kupinga vitendo vya utoaji mimba,jambo ambalo limekuwa pia kipaumbele katika kampeni za uchaguzi Marekani.
No comments:
Post a Comment