Wednesday, May 11, 2016

'Ni aibu kubwa', Buhari amjibu Cameron


Image copyrightSTATE HOUSE
Image caption'Ni aibu kubwa' Buhari amjibu Cameron
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema kuwa serikali yake imepigwa na butwaa na matamshi ya kushtua na ya aibu ya waziri mkuu wa Uingereza Bw David Cameron yakwamba Nigeria na Afghanistan ndio mataifa fisadi zaidi duniani.
Rais Buhari ameyasema hayo muda mchache tu baada ya kupata habari hiyo kumhusu waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.
Rais Buhari akizungumza kupitia msemaji wake, Garba Shehu ametaja matamshi ya Cameron kuwa ya aibu na kushtua.
''Kiongozi huyo wa Nigeria anasema labda Cameron alikuwa akizungumzia utawala uliondoka madarakani mwezi Mei mwaka uliopita wa aliyekuwa rais Goodluck Jonathan.
''Buhari alichaguliwa kwa jukwaa la kupamabana na ufisadi.''
''yeye ndiye kifagio cha ufisadi nchini Nigeria.''
Image copyrightAFP
Image caption''Buhari alichaguliwa kwa jukwaa la kupamabana na ufisadi.''
''Usisahau kuwa rais Buhari alialikwa katika kongamano hilo huko London kutokana na jitihada zake ngangari za kupigana na ufisadi, itakuwaje awe mfisadi''aliuliza bwana Shehu.
Muda mchache uliopita, habari zimeibuka zikimuonesha waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron aliyenaswa na kamera katika dhifa ya kusherehekea miaka 90 tangu kuzaliwa kwake malkia Elizabeth akimwambia Malkia
''viongozi wa mataifa mafisadi wakuu duniani wakiwemo viongozi wa Afghanistan na Nigeria mataifa yanayoorodheshwa kuwa mafisadi zaidi kote dunini watakuwa nchini uingereza siku ya Alhamisi kuhudhuria kongamano la kutathmini mbinu za kukabiliana na zimwi la ufisadi''.
Kiongozi wa kanisa la kianglikana askofu mkuu wa Canterbury Justin Welby aliyekuwa na viongozi hao wawili anaonekana akimkumbusha bw Cameron kuwa rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari si mfisadi.
Hata hivyo Cameron anaonekana akiendeleza mada hiyo.

No comments:

Post a Comment