Friday, May 6, 2016

Rolling Stones wamtaka Trump kutocheza muziki wake


Image copyrightAFP
Image captionRolling Stones
Wanamuziki wa The Rolling Stones wamemtaka mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Demokrat Donald Trump kuwacha kucheza muziki wao wakati wa kampeni zake za urais.
Bendi hyo imetoa taarifa ikisema kuwa mgombea huyo wa uraisi hana ruhusa ya kucheza nyimbo zao na wametaka asitishe kufajnya hivyo mara moja.
Bendi ya Rolling Stones haijatoa ruhusa kwa kampeni ya Trump kutumia nyimbo zao na sasa inaitaka kampeni hiyo kukoma kutumia muziki wake mara moja.
Mgombea huyo amekuwa akicheza nyimbo hizo katika mikutano yake ya kampeni kwa miezi kadhaa sasa.Kibao chao kilichovuma mwaka 1969 ''You Cant Always Get What You Want'' kimekuwa maarufu.
Image copyrightGetty
Image captionDonald Trump
Bendi hiyo sio ya kwanza kutoa lalama kama hizo kwa nyota huyo wa runinga na mfanyibiashara.
Mnamo mwezi Februari ,Adele alitoa taarifa akijiondoa katika uhusiano wowote na Trump baada ya kucheza muziki wa nyota huyo ''In The Deep'' katika mikutano yake.
Mwanamuziki huyo alitoa taarifa akiweka wazi kwamba hajampatia ruhusa mgombea huyo kutumia muziki wake kwa kampeni zake za kisiasa.

No comments:

Post a Comment