Wednesday, May 11, 2016


Image result for camera
Waendesha mashtaka katika Umoja wa Falme za Kiarabu wanasema waandishi habari watatu wa michezo wamepatikana na hatia ya kutusi, kutokana na kauli zao katika kipindi kimoja cha televisheni. Shirika la habari la taifa WAM limeinukuu ripoti ya  ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali ikielezea juu ya waandishi hao kuonekana wanahatia, lakini bila ya kuwataja majina. Taarifa hiyo imesema waandishi hao wamepewa adhabu ya vifungo vya nje na kwamba kesi  inayowakabili kuwataka walipe  fidia ya  dirham 201,000 sawa na  dola 55,000 za Marekani itaendelea. Matamshi yao yalihusiana na kandarasi iliyotolewa kwa kampuni moja ambayo haikutajwa. Wakati  likizingatiwa kuwa taifa la kiliberali katika mashariki ya kati ikilinganishwa na mataifa mengine katika kanda hiyo, Umoja wa Falme za Kiarabu una sheria kali kuhusu uhuru wa kutoa maoni katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

No comments:

Post a Comment