Waziri mkuu Uturuki kujiuzulu.
Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu ametangaza kuwa atajiuzulu katika muda wa wiki mbili zijazo wadhifa wa mkuu wa chama tawala na waziri mkuu.
Uhusiano kati ya waziri huyo mkuu na rais Recep Tayyip Erdogan , umedhoofika katika wiki za hivi karibuni.
Uamuzi wa waziri mkuu huyo kujiuzulu unakuja katika wakati wa matatizo nchini Uturuki , ikiwa ni pamoja na kampeni ya kijeshi dhidi ya watu wanaotaka kujitenga, ugaidi, rushwa na ukandamizaji wa vyombo vya binafsi vya habari.
Josh Earnest , msemaji wa Ikulu ya Marekani , White House, amesema mabadiliko hayo hayataathiri ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika mapambano yao dhidi ya kile kinachojulikana kama kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu, linalojulikana kama IS.
Chama tawala cha Haki na Maendeleo kitafanya mkutano wake maalum baadaye mwezi huu kumchagua mrithi wa Davutoglu.
No comments:
Post a Comment