Saturday, May 7, 2016

Moto mkubwa wazuia shughuli za uokoaji Canada.


Image copyrightReuters
Image captionMoto mkubwa waendelea kuwaka Canada
Maafisa nchini Canada wanasema kuwa moto unaoendelea kuwaka katika mji mkuu wa kuzalisha mafuta na vitongoji vyake wa Fort MucMurray utaongezeka maradufu chini ya muda wa masaa 24 yajayo.
Kuta ndefu za miale ya moto zingine zikifikia mita 60 zimezuia watu wanaotaka kuondoka katika maeneo mbalimbali ya mji huo kutorokea usalama.
Image copyrightAFP
Image captionShughuli za uokoaji zatatizwa
Kiwango na gharama ya hasara iliyopatikana kutokana na moto huo haijagharamiwa, lakini Serikali inasema kuwa zaidi ya nyumba 1,600 zimeteketea na kuwa malipo ya bima yatagharimu mabilioni ya dola.
Maeneo mawili ya kuzoa changarawe yametishiwa na moto huo, ambao umesambaa katika eneo linalozidi ekari 100,000.

No comments:

Post a Comment