Ushemeji wa Mhagama, Tanzanite One wamtia matatani Mbunge Millya.
May 25 2016 tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine, moja ya habari kubwa ni kutoka Gazeti la Jambo Leo lenye kichwa cha habari ‘Ushemeji wa Mhagama, Tanzanite One wamtia matatani Mbunge Millya’.
Gazeti hilo limeeleza kuwa tuhuma za ushemeji kati ya Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenester Mhagama na mmoja wa wabia wa Kampuni ya Sky Associates inayomiliki Mgodi wa Tanzanite One zimelisukuma Bunge kumpa siku nne Mbunge wa Simanjiro ‘CHADEMA’ James Ole Millya athibitishe madai yake kwa ushahidi.
Gazeti hilo limeieleza nukuu ya maneno ya Millya alipokuwa akitoa madai hayo alipokuwa akichangia mjadala bungeni iliyonukuliwa na Naibu Spika, Dk. Tulia ….>>> ‘Sheria za kazi zinajulikana, ni bahati mbaya kwamba Mhagama anatajwa kwamba ni shemeji wa mmoja wa wabia wa hapo. Dada anaitwa Asia Gonga ameolewa na Martin au Yusuph Mhagama’
No comments:
Post a Comment