Wafanyakazi wataka Waziri aondolewe.
Wafanyakazi katika wizara inayopambana na rushwa nchini Brazil wameshindikiza kuondolewa kwa waziri wake mpya.
Maandamano hayo yanafuatiwa kutolewa kwa video ambayo Fabiano Silveira anatuhumiwa kusikika akikosoa uchunguzi wa rushwa katika kampuni ya mafuta ya serikali,Petrobras.Juma lililopita waziri wa mipango wa nchi hiyo alilazimishwa kuachia madaraka baada ya kukumbwa na shutuma kama hizo.Viongozi wote hao wawili walichaguliwa baada ya Rais Dilma Rousseff alipoondolewa madarakani.Amekuwa akisisitiza kwa muda mrefu kuwa mashitaka yaliyoundwa dhidi yake ni kwa ajili tu ya kuzuia upelelezi.
No comments:
Post a Comment