Friday, January 29, 2016


Wanaharakati watatu wa haki za binaadamu nchini China wamehukumiwa kifungo jela. Kwa mujibu wa shirika linalopigania haki za binaadamu Amnesty International,wakili,mpigania haki za binaadamu Tang Jingling amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela. Washitakiwa wenzake pia wamehukumiwa kifungo jela, Yuan Xinting amehukumiwa miaka mitatu, na Wang Qingying miaka miwili na nusu. Katika kesi yao iliyosikilizwa katika mji wa Kanton,watuhumiwa hao watatu walishitakiwa kwa makosa ya kusambaza vitabu vinavyozungumzia mapambano bila ya matumizi ya nguvu.Tangu alipoingia madarakani rais Xi Jinping miaka mitatu iliyopita,wapinzani kadhaa wamehukumiwa kutumikia kifungo jela nchini China.

Wanajeshi wawanyanyasa watoto kingono CAR


Image copyrightAFP
Image captionWanajeshi wa Ufaransa
Wanajeshi walinda amani kutoka Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati CAR wamedaiwa kuwanyanyasa kingono watoto wa taifa hilo.
Kulingana na shirika la habari la AP, Mkuu wa maswala ya kibinaadamu Zeid Raad al-Hussein amethibitisha visa sita zaidi vya unyanyasaji dhidi ya watoto vinavyotekelezwa na majeshi ya Ulaya.
Madai hayo ni ya kutoka mwaka 2014 katika kambi ya watu walioachwa bila makao karibu na uwanja wa ndege wa Bangui.
Afisi ya Bw. Al-Hussein imesema kuwa maafisa wa Umoja wa Mataifa waliwahoji wasichana watano na mvulana mmoja.
Msichana mmoja wa miaka 7 na mvulana wa miaka 9 walisema kuwa waliowanyanyasa walikuwa wanajeshi wa Ufaransa.
Wasichana wengine walidai kwamba waliowanyanyasa walitoka katika kikosi cha kulinda amani cha Georgia.
AP imesema kuwa bw.al-Hussein aliwasilisha malalamishi hayo katika mamlaka za Ulaya,Goergia na Ufaransa pamoja na taifa moja wiki iliopita.

Image result for Donald Trump
Mgombea mmojawapo wa kiti cha rais kutoka chama cha Republican nchini Marekani,Donald Trump ametekeleza aliyoyasema na hakushiriki katika mjadala wa televisheni wa wagombea wa chama hicho kabla ya zoezi la kwanza la kumchagua mgombea wa chama hicho. Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Fox News,kilichoandaa mjadala huo,Trump alitaka alipwe dala milioni 5 ili kushiriki katika mjadala huo. Alitaka fedha hizo zitiwe katika fuko la wakfu wake. Kituo cha Fox News kimeyakataa madai hayo. Badala ya kushiriki katika mjadala wa televisheni,tajiri huyo mwenye kumiliki majumba alikwenda Moines-mji mkuu wa jimbo la Iowa kukusanya fedha kwa ajili ya wapiganaji wa zamani wa vita. Zoezi la kwanza la kumchagua mgombea wa chama cha Republican katika jimbo la Iowa litafanyika Jumatatu ijayo. Donald Trump anaongoza matokeo ya kura ya maoni ya wananchi kwa upande wa chama hicho.

Burundi
Polisi  nchini Burundi wamesema wamewakamata waandishi habari wawili mashuhuri wa kigeni ,waliokua wakiripoti kuhusu watu wenye silaha wanaoipinga serikali ya nchi hiyo ya Afrika kati. Mwandishi habari wa kifaransa Jean-Philippe Remy ambae ni mkuu wa tawi la gazeti la Le Monde barani Afrika, na mwandishi habari mpiga picha wa Uingereza Phil Moore,wamekamatwa jana mchana. Wote wawili wamekuwa wakiripoti kuhusu eneo hilo kwa miaka sasa na wametunukiwa zawadi kadhaa kwa ripoti zao na picha wanazopiga."Wageni hao wawili wamekamtwa wakiwa pamoja na wahalifu waliokuwa na silaha "taarifa ya wizara ya usalama imesema. Polisi wamesema wamekamata pia kombora,bunduki ya rashasha chapa Kalashnikov na bastola. Mkuu wa habari katika ofisi ya rais Willy Nyamitwe amesema alikuwa akutane na Remy jana jioni na kuthibitisha waandishi habari hao wawili ni miongoni mwa watu 17 waliokamatwa na polisi. Shirika la maripota wa kigeni katika eneo la Afrika Mashariki limesema limeingiwa na wasi wasi mkubwa kutokana na kukamatwa maripota hao 2 wanaoheshimika.
\
Image result for obama
 Rais Barack Obama wa Marekani amehimiza juhudi kubwa zaidi zichukuliwe kuwazuwia wanamgambo wa dola la kiislam wasienee nchini Libya. Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani,rais Obama amemtaka mshauri wake wa masuala ya usalama azidishe makali ya mapambano dhidi ya magaidi nchini Libya na katika nchi nyenginezo. Kabla ya hapo waziri wa ulinzi Ashton Carter alisema wanamgambo wa IS wanajenga kambi za mazoezi nchini Libya na kuwaandikisha pia wapiganaji wa kigeni. Ili kuzuwia kuenea kitisho cha itikadi kali kama kile cha Irak na Syria,Marekani inazingatia mikakati tofauti. Jumatano iliyopita, mwakilishi mmoja wa wizara ya ulinzi ya Marekani-Pentagon alizungumzia kuhusu kuchunguzwa uwezekano wa kuanzishwa opereshini za kijeshi nchini Libya.

Saturday, January 23, 2016

TAARIFA ZIKUFIKIE KWAMBA CLUB YA ( Library and Information Movement Club). INAYOUNDWA NA WANACHUO WA SLADS BAGAMOYO WIKI HII WAMEFANYA ZIARA YAO KATIKA SHULE YA SEKONDARI DUNDA. nia na madhumuni soma taarifa hadi mwisho. 

                             WAKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAO BRANDY MUSHI.




Wanafunzi wa chuo cha ukutubi na uhifadhi nyaraka (SLADS) kupitia Club ya wanafunzi Library and Information Movement Club wameanza ziara zao rasmi katika kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya matumizi na umuhimu wa kutumia maktaba katika kufanikisha shughuli zao, na hii ni ziara yao ya kwanza waliyoifanya katika shule ya sekondari Dunda iliyopo Ukuni bagamoyo. 









                    by reporter wangu wanguvu Brandy.

CASFETA SLADS WAKIIMBA WIMBO WA WEWE NI BWANA KATIKA MKESHA WA KUSIFU NA...

NINAZO PICHA KUMI KUTOKA KANIZA LA KLPT BAGAMOYO SEHEMU AMBAYO MKESHA WA KUSIFU NA KUABUDU ULIFANYIKIA. (OVERNIGHT) jana 22/1/2016.


jana update ambayo ilimake headlines kupitia TINGMUGOA.BLOGSPOT.COM ni hii ya overnight ya kusifu na kuabudu, mkesha huo uliandaliwa na wana CASFETA wa chuo cha SLADS BAGAMOYO, mkesha huo ulikuwa ni wa kujiandaa na kuomba baraka juu ya  mitihani inayoenda kufanywa na wanachuo wa chuo hicho  kuanzia juma tatu ya tarehe 25/0/2016. watu walikuwa ni wengi sana hasa wanachuo wa chuo hicho, mkesaha huo ulimalizika saa kumi usiku na ndipo watu wote wakaelekea majumbani mwao kulala. baadae tembelea ting mugoa kupitia youtube kuangalia video za mkesha huo.









Friday, January 22, 2016

OVER NIGHT YA KUSIFU NA KUABUDU: 

Image result for casfeta tanzania

CASFETA SLADS wameandaa mkesha wa kusifu na kuabudu alimaarufu (over night) utakaofanyika leo tarehe 22/1/2016 katika kanisa la KLPT BAGAMOYO kuanzia saa tatu usiku. unakosaje sasa.

Image result for casfeta tanzania

WARUMU 8: 29.

NJOO TUMSIFU BWANA KWA ROHO NA KWELI NAAMINI UTABARIKIWA.

Thursday, January 21, 2016

Image result for Taliban
Wafanyakazi saba wa kituo maarufu cha televisheni nchini Afghanistan, TOLO wameuawa katika shambulizi la kujitoa mhanga dhidi ya basi dogo walilokuwa wakisafiria. Kamanda wa polisi mjini Kabul Gen. Abdul Rahman Rahimi amesema wanawake wawili walikuwa miongoni mwa waliouawa. Shambulizi hilo limefanyika miezi michache baada ya kundi la Taliban kutangaza kwamba kituo hicho kilikuwa shabaha ya shambulizi la kijeshi. Watu wengine 25 walijeruhiwa katika shambulizi hilo lililotokea karibu ya ubalozi wa Urusi mjini Kabul, ambalo ni la kwanza kukilenga kituo cha habari tangu kuangushwa kwa utawala wa wataliban mwaka 2001. Kundi la Taliban limekiri kuhusika na shambulizi hilo, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter. Mwezi Oktoba, wataliban walikishutumu kituo hicho kutangaza habari zisizo sahihi kuhusu harakati zao katika kuukamata mji wa Kaskazini wa Kunduz, na kutishia kukichukulia hatua ambazo kwa wakati huo hawakuziweka wazi.

Zimbabwe yaharamisha ndoa za watoto


Image copyright
Image captionJamii nyingi za Afrika bado zinashikilia utamaduni wa ndoa za wasichana
Mahakama ya kikatiba nchini Zimbabwe imeharamisha ndoa za kitamaduni za watoto, ikisema kuwa watu walio chini ya umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kuoa au kuolewa.
Watoto wamekuwa wakilazimishwa kwa ndoa za mapema kwa misingi ya kidini sehemu kadha za zimbabwe.
Serikali inasema kuwa asilimia 31 ya wasichana huolewa wakiwa chini ya miaka 18 licha ya hilo kuwa kinyume na katiba iliyotekelezwa mwaka 2013.

Magufuli amsimamisha kazi mkuu wa uhamiaji.


MagufuliImage copyrightStatehouse Tanzania
Image captionIdara ya uhamiaji imekabiliwa na tuhuma za rushwa na utendaji mbovu
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji nchini humo Sylvester Ambokile kupisha uchunguzi katika idara ya uhamiaji.
Taarifa kutoka kwa kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu Gerson Msigwa imesema Bw Ambokile amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma za rushwa, ukusanyaji mbaya wa maduhuli ya serikali, ukiukwaji wa taratibu za manunuzi na utendaji mbovu.
Tuhuma hizo zilibainika wakati waziri wa mambo ya ndani ya nchi Bw Charles Kitwanga alipotembelea idara ya uhamiaji hivi karibuni
Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Utawala na fedha Bw Piniel Mgonja pia amesimamishwa kazi.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema watendaji hao wakuu wa uhamiaji wamesimamishwa kazi mara moja hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.
“Endapo watabainika kutokuwa na makosa Rais ataamua hatima yao,” amesema.
Hayo yakijiri, Dkt Magufuli pia amemrejesha Bw Eliakim Chacha Maswi kuwa katibu tawala wa mkoa wa Manyara, baada ya kuhudumu kipindi kifupi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Bw Maswi alikuwa ameteuliwa kuwa kaimu naibu kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
“Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo kwa lengo la kumtafuta mtu mwenye utaalamu wa kuendeleza kazi iliyofanywa na Bw Maswi,” Bw Sefue amenukuliwa katika taarifa hiyo kutoka ikulu.
Tangu kuchukua madaraka mwezi Novemba mwaka jana, Dkt Magufuli amewasimamisha au kuwafuta kazi maafisa wengi wakuu serikalini.