Wednesday, January 6, 2016

Mshukiwa wa ugaidi ajisalimisha kwa polisi Kenya


Gasere
Image captionMaafisa wa usalama walitoa picha ya Salim Mohamed na wengine watatu Jumanne
Mmoja wa washukiwa wanne wa ugaidi waliokwepa msako wa polisi mjini Mombasa Jumatatu amejisalimisha kwa polisi akisindikizwa na babake.
Mohamoud Salim Mohamed almaarufu Gasere alijisalimisha kwa maafisa wa uchunguzi wa jinai mjini Malindi, kaskazini mwa Mombasa, Jumanne jioni.
Maafisa wa usalama waliambia wanahabari Jumanne kwamba polisi walipata bunduki mbili, vilipuzi na pesa baada ya kuvamia nyumba ambayo wanasema ilikuwa ikitumiwa na Mohamed na wenzake.
Washukiwa hao wengine ni Hussein Omar Said almaarufu Babli, Mohamed Ismael Shosi na Kassim Mohamed Abdallah.
Kamishna wa Jimbo la Mombasa Nelson Marwa amefurahia kujisalimisha kwa mshukiwa huyo.
"Hii ni hatua nzuri ambayo babake kijana huyo alichukua na tunawahimiza wazazi wengine kumfuata kabla ya watoto wao kukabiliwa vikali na silaha,” amenukuliwa na gazeti la Daily Nation.
Maafisa wa usalama wanaamini bunduki mbili zilizopatikana katika nyumba hiyo mtaa wa Majengo zilitumiwa katika visa viwili tofauti kuwashambulia maafisa wa usalama.

No comments:

Post a Comment