Tuesday, January 5, 2016

Watumishi wengine wanne wa TAKUKURU wasimamishwa kwa kusafiri nje ya TZ bila kibali.

Image result for magufuli
Hii nimeipata kutoka power breakfast ya clouds fm. Baadhi ya Wabunge wakwama uwanja wa ndege baada ya kukosa kibali cha Bunge na cha Ikulu kuwaruhusu wasafiri nje ya nchi… Watumishi wengine wanne wa TAKUKURU wasimamishwa kwa kusafiri nje ya TZ bila kibali, kuna stori pia kuhusu nauli za mabasi ya mwendokasi kuonekana ni mzigo kwa wananchi, ziko mara mbili ya nauli za sasa.
Mtoto wa Mstaafu wa Polisi Kamanda Kova adaiwa kuhusika na upotevu wa makontena ya bandarini, wataalamu wa tiba toka Hispania wasema wamegundua tiba ya Virusi vya UKIMWI, iko pia taarifa ya msaidizi wa IGP Mangu kufariki kwa ajali ya gari na familia yake Dodoma.
Rais Magufuli amwagiza Mkaguzi mkuu CAG Profesa Assad kuongeza pato la Taifa kutoka 14% ya sasa, shule nyingi za msingi zaonekana kutopokea fedha za kujikimu ili agizo la elimu bure litimizwe.
Ujenzi wa barabara njia nne kuanza Mwanza kutokana na ongezeko la magari.

No comments:

Post a Comment