Mahakama yaidhinisha wagombea urais Niger.
Mahakama ya katiba nchini Niger jana imeidhinisha wagombea 15 wa urais katika uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao. Miongoni mwao ni kiongozi wa kisiasa na mpinzani Hama Amadou, ambaye alifungwa miezi miwili iliyopita baada ya kurudi uhamishoni alikokuwa kwa zaidi ya mwaka mzima. Kuna uwezekano wa mahakama ya katiba kukishinikiza chama tawala kumuachia huru Amadou, ambaye anatarajiwa kuwa miongoni mwa wagombea watatu watakaoongoza katika uchaguzi huo wa Februari 21. Maafisa nchini Niger walimkamata Amadou mwezi Novemba, katika uchunguzi uliohusisha genge linalotuhumiwa kuwachukua watoto wachanga kutoka kile kinachoelezwa kama "viwanda vya kuzalisha watoto" katika nchi jirani ya Nigeria.
No comments:
Post a Comment