Thursday, January 7, 2016

Mshukiwa wa ugaidi afungwa miaka 20 Kenya


Wabwire
Image captionBw Wabwire (aliyejifunika kichwa) akiwa kizimbani
Mshukiwa wa ugaidi aliyeshtakiwa kuwaingiza watoto katika kundi la al-Shabab amehukumiwa kufungwa jela miaka 20 na mahakama Mombasa.
Samuel Wanjala Wabwire almaarufu Salim Mohammed alishtakiwa kuwapa watoto mafundisho ya itikadi kali.
Alikuwa ameshtakiwa pia kuwa mwanachama wa kundi hilo kutoka Somalia.
Watoto waliotoa ushuhuda kwenye kesi yake wanasema aliwafunza kwamba Wakristo ni makafiri ambao wanafaa kuuawa.
Baadhi ya watoto hao walisilimu.
Bw Wabwire alikuwa mwalimu wa shule ya msingi na pia imam katika Masjid Jihad.
Alikabiliwa pia na shtaka la tatu la kueneza itikadi kali na vita vya kidini. Anadaiwa kutoa mafunzo ya karate msikitini.
Alikamatwa mwezi Juni mwaka 2015 eneo la Kaloleni, jimbo la Kilifi.

No comments:

Post a Comment