Friday, January 29, 2016

Wanajeshi wawanyanyasa watoto kingono CAR


Image copyrightAFP
Image captionWanajeshi wa Ufaransa
Wanajeshi walinda amani kutoka Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati CAR wamedaiwa kuwanyanyasa kingono watoto wa taifa hilo.
Kulingana na shirika la habari la AP, Mkuu wa maswala ya kibinaadamu Zeid Raad al-Hussein amethibitisha visa sita zaidi vya unyanyasaji dhidi ya watoto vinavyotekelezwa na majeshi ya Ulaya.
Madai hayo ni ya kutoka mwaka 2014 katika kambi ya watu walioachwa bila makao karibu na uwanja wa ndege wa Bangui.
Afisi ya Bw. Al-Hussein imesema kuwa maafisa wa Umoja wa Mataifa waliwahoji wasichana watano na mvulana mmoja.
Msichana mmoja wa miaka 7 na mvulana wa miaka 9 walisema kuwa waliowanyanyasa walikuwa wanajeshi wa Ufaransa.
Wasichana wengine walidai kwamba waliowanyanyasa walitoka katika kikosi cha kulinda amani cha Georgia.
AP imesema kuwa bw.al-Hussein aliwasilisha malalamishi hayo katika mamlaka za Ulaya,Goergia na Ufaransa pamoja na taifa moja wiki iliopita.

No comments:

Post a Comment