Wawili wauawa katika tetemeko India.
Watu wasiopungua wawili wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika tetemeko la ardhi lilitokea kaskazini-mashariki mwa India, karibu na mpaka wa Myanmar. Katibu mkuu wa jimbo la Manipur Sureshi Babu, amesema vifo viwili vimeripotiwa katika mji wa Imphal pamoja na majeruhi, lakini akaongeza kuwa hawawezi kusema kwa uhakika idadi ya watu waliojeruhiwa kwa sababu bado hawajapata taarifa kutoka maeneo ya ndani. Amesema pia majengo mawili yaliyokuwa yanajengwa yameporomoka mjini humo, lakini hakuna aliekwama. Sureshi Babu amesema uharibifu na vifo kutokana na tetemeko hilo havikuwa vikubwa kama ilivyohofiwa, kwa sababu ya majengo mafupi, na kwa kuwa limetokea katika eneo ambalo halina msongamano wa wakaazi.
No comments:
Post a Comment