Merkel akataa kusalimu amri kuhusu wakimbizi.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametilia mkazo upinzani wake dhidi ya kuweka ukomo kwa idadi ya wahamiaji na wakimbizi wanaoruhusiwa kuingia nchini humo, wakati akijaribu kutuliza wasiwasi ndani ya muungano wake katika mkuu wa chama mshirika. Merkel amekuwa akikwaruzana na kiongozi wa chama ndugu cha Christian Social Union CSU, Horst Seehofer, kuhusiana na mapendekezo yake ya kuruhusu kiwango cha juu kabisaa cha wahamiaji laki mbili kuingia Ujerumani mwaka huu. Merkel alisema kuna misimamo inayotofautiana, na hilo lisingeweza kubadilika katika mkutano wa CSU, uliyofanyika katika eneo la kitalii la Wildbad Kreuth katika jimbo la Bavaria. Wakati amesisitiza kuwa yeye pia anataka kuona idadi ya wahamiaji wanaowasili ikipungua, lakini alikataa kuunga mkono pendekezo la CSU.
No comments:
Post a Comment