Taliban yauwa wafanyakazi 7 wa kituo cha habari Kabul.
Wafanyakazi saba wa kituo maarufu cha televisheni nchini Afghanistan, TOLO wameuawa katika shambulizi la kujitoa mhanga dhidi ya basi dogo walilokuwa wakisafiria. Kamanda wa polisi mjini Kabul Gen. Abdul Rahman Rahimi amesema wanawake wawili walikuwa miongoni mwa waliouawa. Shambulizi hilo limefanyika miezi michache baada ya kundi la Taliban kutangaza kwamba kituo hicho kilikuwa shabaha ya shambulizi la kijeshi. Watu wengine 25 walijeruhiwa katika shambulizi hilo lililotokea karibu ya ubalozi wa Urusi mjini Kabul, ambalo ni la kwanza kukilenga kituo cha habari tangu kuangushwa kwa utawala wa wataliban mwaka 2001. Kundi la Taliban limekiri kuhusika na shambulizi hilo, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter. Mwezi Oktoba, wataliban walikishutumu kituo hicho kutangaza habari zisizo sahihi kuhusu harakati zao katika kuukamata mji wa Kaskazini wa Kunduz, na kutishia kukichukulia hatua ambazo kwa wakati huo hawakuziweka wazi.
No comments:
Post a Comment