Uganda yashutumiwa kubana uhuru wa kujieleza kueleleka uchaguzi.
Shirika la kutetea haki za binadaamu la Human Rights Watch limesema vitisho vya serikali ya Ugandadhidi ya vyombo vya habari na wanaharakati vimeathiri vibaya uhuru wa kujieleza nchini humo, miezi michache kabla ya uchaguzi utakaofanyika tarehe 18 Februari.
Wagombea saba wa upinzani wanawania kuufikisha mwisho utawala wa miaka 30 wa Rais Yoweri Kaguta Museveni na kuna hofu ya kuwa kampeni za uchaguzi huo zitakumbwa na ghasia, huku kila upande ukiushutumu mwingine kuwapa silaha wanamgambo katika kuwania madaraka.
Ripoti ya Human Rights Watch iliyochapishwa leo, imesema waandishi kadhaa wamesimamishwa kazi kutokana na shinikizo la serikali, na kwamba vituo vya redio vilivyowahoji wanasiasa wa upinzani wenye kutoa maoni yanayokipinga chama tawala, vimetishwa. Katika ripoti hiyo iliyopewa jina, 'Wanyime watu Taarifa'' Human Rights Watch imesema uchaguzi wa haki unahitaji nafasi sawa kwa wagombea wote kunadi sera zao kwa wapiga kura.
No comments:
Post a Comment