Friday, January 29, 2016


Burundi
Polisi  nchini Burundi wamesema wamewakamata waandishi habari wawili mashuhuri wa kigeni ,waliokua wakiripoti kuhusu watu wenye silaha wanaoipinga serikali ya nchi hiyo ya Afrika kati. Mwandishi habari wa kifaransa Jean-Philippe Remy ambae ni mkuu wa tawi la gazeti la Le Monde barani Afrika, na mwandishi habari mpiga picha wa Uingereza Phil Moore,wamekamatwa jana mchana. Wote wawili wamekuwa wakiripoti kuhusu eneo hilo kwa miaka sasa na wametunukiwa zawadi kadhaa kwa ripoti zao na picha wanazopiga."Wageni hao wawili wamekamtwa wakiwa pamoja na wahalifu waliokuwa na silaha "taarifa ya wizara ya usalama imesema. Polisi wamesema wamekamata pia kombora,bunduki ya rashasha chapa Kalashnikov na bastola. Mkuu wa habari katika ofisi ya rais Willy Nyamitwe amesema alikuwa akutane na Remy jana jioni na kuthibitisha waandishi habari hao wawili ni miongoni mwa watu 17 waliokamatwa na polisi. Shirika la maripota wa kigeni katika eneo la Afrika Mashariki limesema limeingiwa na wasi wasi mkubwa kutokana na kukamatwa maripota hao 2 wanaoheshimika.

No comments:

Post a Comment