Ubalozi mdogo wa India Mazar-i-Sharif washambuliwa.
Ubalozi mdogo wa India nchini Afghanistan umeshambuliwa na watu waliojihami kwa silaha, ambao idadi yao haikujulikana mara moja. Hakujatolea taarifa juu ya idadi ya walioathirika katika shambulio hilo au hasara iliyopatikana, lakini afisa wa ubalozi huo aliwambia waandishi habari kwamba wafanyakazi wote wa ubalozi walikuwa salama.
Shambulizi hilo limekuja siku chache baada ya waziri mkuu wa India Narendra Modi, kufanya ziara mjini Kabul, na kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Pakistan Nawazi Sharif. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo.
No comments:
Post a Comment