Viwanda vya makaa ya mawe Ujerumani hutoa Zebaki nyingi.
Imebainika kuwa viwanda vinavyofua umeme kwa kutumia makaa ya mawe vinatoa tani mbili zaidi za madini ya zebaki kuliko ilivyodhaniwa hapo awali. Hii inafuatia utafiti uliofanywa na taasisi ya masuala ya tekolojia na siasa ya mjini Hamburg nchini Ujerumani. Na ingawa Ujerumani inatazamwa mara nyingi kama nchi rafiki wa mazingira, zaidi ya asilimia 40 ya mahitaji ya nishati ya nchi hiyo yanatokana na umeme wa makaa ya mawe. Waziri wa mazingira wa Ujerumani Barbara Hendrick amazungumzia utafiti huo kwa kusema Ujerumani lazima iachane na umeme wa makaa ya mawe ili kutimiza malengo ya muda mrefu ya tabianchi. Zebaki imeonyesha kusababisha matatizo kadhaa, yakiwemo saratani na kuharibu mfumo wa neva.
No comments:
Post a Comment