Waziri mkuu Cote D'voire ajiuzulu na baraza lake.
Waziri mkuu wa Cote D'voire Daniel Kablan Duncan na serikali yake wamejiuzulu jana Jumatano. Hatua yake imekuja baada ya rais kuelezea nia yake ya kuongeza ufanisi katika serikali, wakati taifa hilo likipambana kutekeleza mageuzi. Taifa hilo la Afrika Magharibi limeshuhudia ukuaji wa kasi wa uchumi, lakini watu wengi wamesema hawajanufaika na ukuaji huo. Rais Alassan Outtara amekubali kujiuzulu kwa waziri mkuu na baraza lake.
No comments:
Post a Comment